Sekta ya mafuta ya mawese nchini Malaysia inatatizika kufuata kanuni za Umoja wa Ulaya


Udhibiti mpya wa EU unalenga kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa kadhaa, ikiwa ni pamoja na mafuta ya mawese, ambayo yanatoka kwenye mashamba yanayohusishwa na ukataji miti. Wakati umoja huo ukisifu sheria hiyo kama njia muhimu ya kulinda misitu duniani, nchi za Kusini Mashariki mwa Asia zinasema inatishia maisha yao na ni vigumu kuitekeleza. Malaysia ni mojawapo ya wazalishaji wakuu wa mafuta ya mawese duniani na wakulima huko wana wasiwasi wanaweza kupoteza mapato yao. Timu yetu inaripoti kutoka kisiwa cha Borneo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *